Sunday, June 11, 2017

Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha 5 na Vyuo vya Ufundi awamu ya Kwanza 2017

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha Tano Mwaka 2017


1.0 UTANGULIZI

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)
kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
imekamilisha zoezi la uchaguzi na upangaji wa wanafunzi wa kujiunga
na masomo ya Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi vya Serikali kwa
mwaka 2017 ambao walihitimu Kidato cha Nne mwaka 2016.
 

2.0 MATOKEO YA UFAULU KWA UJUMLA 
Jumla ya watahiniwa wa shule 349,524 wakiwemo wasichana 178,775sawa na asilimia 51.1 na wavulana 170,749 sawa na asilimia 48.9walifanya mtihani wa kumaliza Kidato cha Nne mwaka 2016. Watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani huo mwaka 2016 walikuwa 47,751 wakiwemo wasichana 24,587 sawa na asilimia 51.5 na wavulana 23,164 sawa na asilimia 48.5.Watahiniwa waliofaulu kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara. Hivyo ufaulu katika mwaka 2016 uliongezeka kwa asilimia 3.15ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2015.
 
3.0 TARATIBU ZA UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI KWA MWAKA 2017
Kwa mujibu wa mwongozo wa uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano, mwanafunzi anayeomba kuchaguliwa kuendelea na Elimu ya Sekondari ya Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi hulazimika kujaza fomu ya uchaguzi Selform ambayo ndiyo fomu rasmi ya maombi ya kuchaguliwa. Kwa kutumia fomu hiyo, mwanafunzi hujaza machaguo matano ya tahasusi (Combinations) za masomo anayotaka kusoma na Shule anayoipenda kujiunga nayo kwa kila chaguo.
Kwa kuzingatia utaratibu huo, Mfumo wa kieletroniki wa Uchaguzi hutumika kumpanga mwanafunzi katika machaguo yake ya masomo na Shule kwa kuanzia na chaguo la kwanza hadi la tano kulingana na kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi. Mfumo humpangia mwanafunzi chaguo la tahasusi aliyofaulu zaidi kuliko machaguo mengine.
Kwa mwaka huu 2017 Uchaguzi na upangaji wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi umezingatia mwongozo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wa tarehe 15 Mei, 2017. Mwongozo huu unaelekeza kwamba, kigezo cha mwanafunzi kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi ni;
i)
AAA hadi CCD kama cut off point kwenye masomo ya tahasusi
ii) Credit 3 na pointi zisizopungua
25 kwenye Daraja,
iii) Machaguo yaliyojazwa na mwanafunzi kwenye selform. 
iv) Nafasi zilizopo katika Shule husika
Napenda kusisitiza kwamba, vigezo hivi ndivyo vinavyotumika kwa mwanafunzi kujiunga Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka huu. Nia ni kuinua kiwango cha Elimu na Ujuzi kwa Elimu ya Juu Nchini.
 

4.0 WANAFUNZI WENYE SIFA ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO MWAKA 2017
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha Tano mwaka 2017wanatoka kwenye Shule za Serikali na zisizo za Serikali ambapo Shule351 zikiwemo shule 17 mpya zimepangiwa wanafunzi.
Kati ya wanafunzi 96,018 ni wanafunzi
93,019 ndio wenye sifa za kuchaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa kuwa wamefaulu vigezo vyote vya msingi kama nilivyoainisha hapo juu. Kati ya hao, Wanafunzi 92,998 ni wa Shule (School Candidates) na Wanafunzi 21walisoma chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima. 

 5.0 TAREHE YA KURIPOTI WANAFUNZI KATIKA SHULE WALIZOPANGIWA 
Muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano kwa mwaka 2017, utaanza tarehe 17 Julai 2017 lakini kwa wanafunzi wanaongia Kidato cha Sita watafungua Shule tarehe 3/7/2017 kama ilivyokuwa imepangwa. Kwa kuwa upangaji wa wanafunzi wanaoingia Kidato cha Tano kwa mwaka 2017 umezingatia machaguo ya wanafunzi wenyewe na nafasi zilizopo katika Shule husika, hakutakuwa na fursa ya kufanya mabadiliko yoyote ya Shule.Nitumie nafasi hii, kuwaagiza wanafunzi wote kuripoti katika Shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya kufungua Shule , nafasi yake itachukuliwa na wanafunzi wengine.
 

Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2017 inapatikana kwenye tovuti ya ORTAMISEMI ya: www.tamisemi.go.tz & www.moe.go.tz 
Aidha, fomu za kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi (joining instructions) zinapatikana kwenye shule alikopangiwa mwanafunzi na kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ya: www.tamisemi.go.tz





  

CLICK/BONYEZA HAPA KUPATA JOIN INSTRUCTIONS KIDATO CHA TANO 2017/18 >>>  
    







3 comments:

  1. Tanzania ni nchi isyokuwa na uhak na usawa acheni kudhulumu kusoma kazi mi nina three ya 23 sirusiwi kwenda kidato cha tano na kama mmsema mwenye daraja la Kwanzaa hadi la Tatu ndo waliochaguliwa je mm na wengne mliotuacha na tuna three tena tahasusi zetu zmebalansi na mmetuacha nia yenu ipi mi nasoma na walim watano shulen kwa idadi hiyo ya walim najituma mpaka nmefaulu mwisho wa sku mmnaniacha na wakati mmwachukua watu wenye three ya 25 tena tahasus haijabalanc dah haki sawa kwa Kila mtanzania hamjatutendea jaman kaeni China mjua mnatusaidiaje tutaenda wapi na three zetu mazngra tuliyosomea magumu walimu watanooooooo asanteni ukiipata meseji hii isambaze ifke kwa wahusika jaman

    ReplyDelete
  2. Inauma sana kila nikiwaza walim Akuna nimetumia hela nyingi tusheni lengo nmefaulu niendelee mbele matokeo yanakuja nmefaulu nasubiri usajili unakuja sijasajiliwa na wametangaza kuwa mwenye three ya kuanzia daraja la 1had3 wanachukuliwa ss tupo wapi HAKI NA USAWA HAMJATUTENDEA basi mungetangaza tu kama huna division two na one hautochukuliwa mpaka leo tungekuwa hata kurudia shule mapema jaman

    ReplyDelete
  3. Hujambo Kiba Abeid? Tafadhali angalia ORODHA YA WATAKAOPANGIWA SECOND SELECTION Kama jina lako lipo. Hakuna mwanafunzi mwenye sifa atakayeachwa. Iamini serikali yako. Wizara imetoa list ya watakaopangiwa awamu ya pili na michepuo watakayopangiwa.

    ReplyDelete