MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI MKUU
Shule ya Sekondari Mkuu ni shule
nzuri ambayo ni mchanganyiko kuanzia Kidato cha I – IV. Wanafunzi wa kidato cha tano na sita ni wasichana tu.
Wanafunzi wote wasichana wa kidato cha tano na sita wanakaa kwenye mabweni yaliyopo shuleni. Wanafunzi wa kidato cha 1 - 4 wanalala nyumbani.
Shule ya Sekondari Mkuu iko katika mazingira mazuri ya mwanafunzi kusoma na kuweza kufaulu vizuri kama ataonyesha bidii ya kusoma. Shule inao walimu wa kutosha na huduma zote muhimu kwa wanafunzi zipo shuleni. Mwanao aitumie nafasi hii aliyopewa na Serikali vizuri baadaye alisaidie Taifa letu, wazazi wake na yeye mwenyewe kwa siku za baadaye akizingatia kwamba wenzake wengi hawakuchaguliwa.
Kwa ushindi huo wa mwanao tunawapongeza wewe mzazi pamoja na mwanao kwa kuchaguliwa kwake.
Wanafunzi wote wasichana wa kidato cha tano na sita wanakaa kwenye mabweni yaliyopo shuleni. Wanafunzi wa kidato cha 1 - 4 wanalala nyumbani.
Shule ya Sekondari Mkuu iko katika mazingira mazuri ya mwanafunzi kusoma na kuweza kufaulu vizuri kama ataonyesha bidii ya kusoma. Shule inao walimu wa kutosha na huduma zote muhimu kwa wanafunzi zipo shuleni. Mwanao aitumie nafasi hii aliyopewa na Serikali vizuri baadaye alisaidie Taifa letu, wazazi wake na yeye mwenyewe kwa siku za baadaye akizingatia kwamba wenzake wengi hawakuchaguliwa.
Kwa ushindi huo wa mwanao tunawapongeza wewe mzazi pamoja na mwanao kwa kuchaguliwa kwake.
USAFIRI WA KUJA SHULENI
Mwanafunzi akifika moshi mjini stendi kuu ya mabasi akitokea popote pale, uliza na apande magari yaendayo Rombo kupitia Mwika hadi Tarakea. Shule yetu ipo umbali wa kilomita 60 kutoka Moshi mjini hadi Mkuu Rombo kabla hujafika Tarakea. Nauli ya kutoka Moshi mjini hadi Mkuu Rombo ni Tshs. 4000/= hadi Tshs. 5000 kutategemeana na gari. Kwa wanafunzi wanaotoka Dar es Salaam au kupitia DSM wapande magari ya Dar express, Meridian, Esther coach, Saibaba, Metro coach, Tilisho Coach yanayokuja moja kwa moja Rombo. Kwa Kutokea Dodoma panda bus la Shabibi au Ngasere linalokuja moja kwa moja Rombo. Wanaotokea Singida panda bus la Mtei Express la Rombo. Na kutokea Mwanza panda bus la Mghamba.KITUO CHA KUTEREMKIA
Ukitokea Moshi mjini mwambie kondakta wa gari utateremkia Mkuu-Kanisani vilevile kwa wale wanaotokea Tarakea kuelekea Moshi nao watateremkia Mkuu-kanisani. Kutoka hapo Mkuu-Kanisani kuelekea shuleni ni umbali wa mita 150 utakuwa umefika shuleni.
Ukifika shuleni utaripoti na kupokelewa na mwalimu wa zamu au Makamu wa Mkuu wa shule ambao wote watakuwepo shuleni kwa kipindi hicho. Baada ya kuripoti shuleni utasajiliwa ofisini kwa Makamu wa Mkuu wa shule ukiwa na mahitaji yote muhimu uliyoagizwa kuleta shuleni.
HUDUMA ZINAZOPATIKANA SHULENI
Shule inalo duka ambalo hutoa huduma za mahitaji karibu yote muhimu kwa wanafunzi na watumishi wote wa shule. zahanati ya Mission Mkuu iko karibu na shule. Hospitali kubwa ya Wilaya ipo karibu na shule ina gari, usafiri wa kuja shuleni na kurudi nyumbani ni mzuri kwani shule ipo karibu sana na barabara, Benki, Posta vyote viko karibu.MIRADI YA SHULE:
Shule
yetu inayo miradi kama ifuatayo ambayo huhudumiwa na wanafunzi na baadhi ya
watumishi ambao vile vile hutumika kwa mafunzo:-
1.
Duka la shule
2.
Ng’ombe wa maziwa
3.
Bustani ya mboga
4. Mgahawa
5.
Shamba la migomba
Download>>>FORM ONE 2024 Joining Instuctions
Download>>>FORM FIVE 2024/2025 Joining Instructions
Mwisho tunampongeza tena
mwanao kwa kuchaguliwa kwake na tunamkaribisha
Shule ya Sekondari Mkuu.
KARIBU
SANA.
Kazi nzuri sana, mmekuwa wa kisasa, keep it up
ReplyDeleteBig up
DeleteEnter your comment...hakuna bwen kwa boys
ReplyDeleteKama ilivyoelezwa hapo juu. Kwa O-level wanafunzi ni wa kutwa. Na kwa A-level wanafunzi ni wa bweni tena wakike tu!
DeleteVilevile kwa O-level kuna private hostel za kike na kiume zinazomilikiwa na kanisa (parokia ya Mkuu).
ninaomba msaada wa taratibu za kumleta mtoto O-level. nimekuwa interested sana na namna shule inafanya vizuri na ipo kisasa katika huduma zake.
ReplyDeleteShule hii ni ya serikali. Wanafunzi hupangiwa hapa na serikali. Ukitaka kumleta mwanao ambaye hajapangiwa hapa itakubidi kufuata taratibu za uhamisho wa mwanafunzi...
DeleteAsante kwa maelekezo mazuri na ushauri 1. naweza kupata namna ya mawasianiano na ofisi ya taaluma kama kujua nafasi kama zipo na taratibu hizo za kuhamisha mtoto?. naomba msaada tafadhali.
ReplyDeleteNamba za uongozi wa shule tembelea link hii:
ReplyDeletehttps://mkuutaaluma.blogspot.com/p/contact-us.html
Sorry, the page you were looking for in this blog does not exist. Mine coins - make money: http://bit.ly/money_crypto
ReplyDeleteMine coins - make money: http://bit.ly/money_crypto
najibiwa hivyo. But shida yangu kubwa ni kufahamu kama nafasi zipo na naweza kufanya utaratibu wa kumleta mtoto
Je hapo shuleni unaruhusiwa kubadili combination Kama una qualifications?
ReplyDeleteNdio. Tofauti na kuwa na vigezo, pia itategemea na maelekezo yatakayotolewa mwaka huu kuhusu kubadili Comb.
DeleteKuna na fasi kwa walewakurudia mtiani wa form four
DeleteHongera mkuu secondary kwa kutoa huduma nzuri
ReplyDeleteTunashukuru sana.
DeleteJoining instruction ya mwaka huu kwa form five iko tayari?
ReplyDeleteNdio, ipo tayari. waweza kudownload kwa kupitia link iliyopo hapo juu.
DeleteHizo private hostel za kanisa naelewa ni za kulipia. Ningeomba kujua no sh ngapi?je mwanafunzi wa A level anaruhusiwa kutumia
DeleteNi kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne. Wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 wanalala bweni la shule.
DeleteGharama za hostel ya kanisa ni 600,000 kwa mwaka.
Herini sana kwa mwaka mpya na hongereni kwa kazi nzuri mnayofanya hapo.
ReplyDeleteTafadhali naomba kuuliza swali.Wanafuzi waliokuwa kidato cha pili wanaotarajiwa kuingia kidato cha tatu mwaka huu 2021 ni categories gani zinaendelea wakati matokeo bado hayajatoka?Je wanaendelea kuja shuleni au kuna uaratibu mwingine uliotolewa wa kusubiri matokeo ya kidato cha pili yatoke?maana watu wamekuwa njia panda kuhusu matokeo kutotolewa kwa wakati.
Ninatumaini mtakuwa na fununu juu ya hili japo haijawekwa wazi kama matokeo yatatoka lini!Otherwise mkute mliwapa taarifa kama wasubirie matokeo yakishatoka ndio waende shule.Asante sana naomba kuwasilisha.
Tunaomba joinning instaction za mwaka huu
ReplyDeletejoining instruction za form5 mwaka huu mbn hazipo online
ReplyDeleteTuwekeeni join instruction ya form Five ya 2021
ReplyDeleteZipo. Jaribu kudownload tena. Wameshaweka.
ReplyDeleteMeanangu nataka nimwamishie hapo naomba utararatibu na namba za muhusika ili anielekeze jinsi nitakavyo fatilia uhamisho prem no na vitu vingine ataanza kidato Cha kwanza 2022
ReplyDeletehttps://mkuutaaluma.blogspot.com/p/contact-us.html
DeleteNaomba form za kujiunga form 5 2022/2023
DeleteForm za kujiunga na form 5 tayari?
ReplyDeleteTayari. Bonyeza link hapo juu kuDownload.
DeleteAhsante
ReplyDeleteMwisho was tarehe ya kuripoti ni lini?
ReplyDeleteMwisho wa tarehe ya kuripoti ni lini?
ReplyDeleteOk yumeielewa je? Gorm zinajzwa shuleni au uku nyumbn
ReplyDeleteTumeelewa vizur je? Form inatakiwa kujazwa shulen.au nyumbn
ReplyDeleteMwanafunzi anapaswa kuriport akiwa na form iliyojazwa kikamilifu.
DeleteWaaoon wonderful I like my schol
ReplyDeleteHongereni Mkuu Sekondari Kwa kazi nzuri ya utoaji elimu Kwa vijana wa kitanzania. Naomba kufahamu Kuna huduma ya bweni Kwa o-level both girls and boys Kwa mwaka 2023?
ReplyDeleteAsante. Hakuna huduma ya bweni kwa O-Level. Ila kuna huduma ya hostel binafsi inayotolewa na Parokia ya Mkuu kwa wanafunzi wa O-level wanaotaka kukaa hostel.
DeleteJe mnapokea wanafunzi wanaohamia
ReplyDeleteNdio
DeleteTunazipataje za kidato Cha tano
DeleteBonyeza link hapo juu utaweza ku-download
DeleteJoin instructions za mwaka huu zipo tayari!??
ReplyDeleteHabari? Join instructions zipo tayari. Bonyeza link hapo juu.
DeleteMkuu secondary school
ReplyDeleteHabari, naomba utaratibu namna ya kupata hizo hostel za parokia Kwa wanafunzi wa o level, ikiwezekana na mawasiliano Yao pia
ReplyDeleteSamahani naomba kuuliza nitapata nafasi ya mwanafunzi wa kidato cha tano anasomea HGK naombeni mnisaidie
ReplyDeleteShule haina tahasusi hiyo ya HGK.
Deletenauliza maksi za wasichana join form 5 ni ngapi
ReplyDeleteWanafunzi wanasuka au wananyoa wa A level kwenye join instructions akuna about that
ReplyDeleteSoma ukurasa wa tano, kipengele cha Vi.
Delete