Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania anawatangazia watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato Cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) Mwezi Novemba 2015 kwamba usajili umeanza rasmi tarehe 01 Januari 2015.
Watahiniwa watakaojisajili katika kipindi cha kawaida yaani tarehe 01 Januari 2015 hadi 28 Februari 2015 watalipa ada ya Shilingi 50,000/- kwa wanaojisajili mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Shilingi 30,000/- kwa wanaojisajili mtihani wa Maarifa (QT).
Watahiniwa watakaojisajili kwa kuchelewa yaani kuanzia tarehe 01 Machi 2015 hadi tarehe 31 Machi 2015, watalipa ada ya Shilingi 65,000/ kwa Kidato cha Nne na ada ya Shilingi 40,000/- kwa mtihani wa Maarifa (ada pamoja na faini).
Kabla ya kujisajili kwenye mtandao waombaji watapaswa kwenda kwenye vituo wanavyokusudia kufanyia mtihani kuchukua namba rejea (Reference Number). Wakuu wote wa vituo nchini wamekabidhiwa namba rejea na watazigawa kwa watahiniwa tarajali bila malipo. Aidha waombaji watapaswa pia kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au M-Pesa kabla ya kujisajili kwani hakuna mtahiniwa atakayeweza kujisajili bila kulipa ada ya mtihani. Waombaji wote wazingatie kwamba kipindi cha usajili kitafungwa rasmi tarehe 31 Machi 2015. (kwa maelezo zaidi kutoka baraza la mitihani la Tanzania, Bofya HAPA au tembelea www.necta.go.tz)
Shule ya sekondari Mkuu, ni kituo kwa watahiniwa wa kujitegemea wa Maarifa (QT), Kidato cha nne(CSEE) na kidato cha sita(ACSEE). Kituo hiki cha watahiniwa wa kujitegemea kinasimamiwa na Taasisi ya Elimu ya watu wazima (TEWW/IAE) chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Kituo kimesajiliwa kwa namba M0544 na P0544. Kituo kinatoa elimu kwa wanaohitaji kuanzia muda wa jioni saa 9, kwani kituo hiki kina walimu bora na waliobobea katika kutoa elimu na ushauri kwa wale wanaorudia na kwa wale wanaojiendeleza.
Karibu/Karibuni sana katika Kituo cha Shule ya Sekondari Mkuu.
Ukifika, Ulizia mratibu wa Watahiniwa wa kujitegemea(PC), Au Mwalimu Tarimo au Makamu Mkuu wa Shule. Utapata maelekezo ya namna ya kulipa ada ya mtihani na kujisajili, na kama utakuwa tayari basi utasajiliwa hapohapo. Endapo utapenda kujiunga kusoma katika kituo cha shule ya sekondari Mkuu, utapatiwa fomu ya kujiunga na kituo hiki.
No comments:
Post a Comment