Saturday, January 9, 2016

USAJILI WA WATAHINIWA WA KUJITEGEMEA KIDATO CHA SITA (ACSEE) 2017

Tunapenda kuwajulisha watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) mwezi MEI, 2017 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba; 

1. Kipindi cha usajili kwa watahiniwa wa Kujitegemea kitaanza tarehe 1 Julai hadi 30 Septemba, 2016 kwa ada ya Shilingi 50,000/= Aidha, watakaojisajili kwa kuchelewa yaani tarehe 01/10/2016 hadi tarehe 30/10/2016 watalipa Shilingi 65,000/= ikiwa ni ada ya kawaida pamoja na faini. 

2. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani kuchukua namba rejea (reference number) zinazotolewa bure na kufanya malipo ya ada ya mtihani katika ofisi za Posta tu. 

3. Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz kwani muda wa usajili hautaongezwa.

Shule ya sekondari Mkuu, ni kituo kwa watahiniwa wa kujitegemea wa Maarifa (QT), Kidato cha nne(CSEE) na kidato cha sita(ACSEE). Kituo hiki cha watahiniwa wa kujitegemea kinasimamiwa na Taasisi ya Elimu ya watu wazima (TEWW/IAE) chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Kituo kimesajiliwa kwa namba M0544 na P0544. Kituo kinatoa elimu kwa wanaohitaji  kuanzia muda wa jioni saa 9, kwani kituo hiki kina walimu bora na waliobobea katika kutoa elimu na ushauri kwa wale wanaorudia na kwa wale wanaojiendeleza.

Karibu/Karibuni sana katika Kituo cha Shule ya Sekondari Mkuu.
Ukifika, Ulizia mratibu wa Watahiniwa wa kujitegemea(PC), Au Mwalimu Tarimo au Mwalimu wa Taaluma. Utapata maelekezo ya namna ya kulipa ada ya mtihani na kujisajili, na kama utakuwa tayari basi utasajiliwa hapohapo. Endapo utapenda kujiunga kusoma katika kituo cha shule ya sekondari Mkuu, utapatiwa fomu ya kujiunga na kituo hiki.

17 comments:

  1. Hii shule iko wapi, naomba kujua tafadhari!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shule ya sekondari Mkuu, ipo katika mkoa wa Kilimanjaro, Wilaya ya Rombo, Tarafa ya Mkuu.

      Delete
  2. ukitokea QT unaweza kufanya mtihani wa kidato cha sita kama school candidate?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndio inawezekana kama utakizi vigezo... Wapo wanaochaguliwa moja kwa moja na serikali kwenda kidato cha tano.

      Delete
  3. Ada ya kituo pc acsee NI sh ngap jumla? Kwa cbg comb

    ReplyDelete
  4. Ada jumla kwa cbg ni shingapi kurudiwa mtihani

    ReplyDelete
  5. Wanaotokea nje ya dar ili kurudia mtihani gharama zote ni shingap

    ReplyDelete
  6. Kama lugha no tatizo kama kingereza je unaweza ukafanya vuzur

    ReplyDelete
  7. Ili niweze kufanya mtihani wa kidato cha sita natakiwa niwe na ufaulu angalau ukovipi

    ReplyDelete
    Replies
    1. 1.Uwe umehitimu kidato cha nne kwa daraja lolote.
      2.Uwe na credits 3 za masomo yoyote uliyofanya kidato cha nne.
      3.Usiwe na F katika masomo ya comb unayotaka kufanya kidato sita. (bali hata ukiwa na F system inakubali ila itakusumbua baadae katika chuo au ajira).

      Kwa maelezo zaidi fika kituoni.

      Delete
    2. Inakuaje kwenye kuapply vyuo vya serikali maana mfano udsm wanasema sifa kujiunga kwao uwe na 3 credit na 2 pass mfano mtu 3 credits na F nyengine atachaguliwa? Akimaliza form six

      Delete
  8. mimi nilimaliza kidato cha sita 2019 mchepuo wa HGL naweza kubadili mchepuo kwenda PCB na nikafanya kama QT.ASANTE

    ReplyDelete
  9. Je ikiwa comb haikubalance naweza kufanya mtihan mfano history D,kiswah c na English C HKL

    ReplyDelete
  10. Nimemaliza chuo grade A nataka kujiendeleza form six matokeo yangu ya form four nina three nataka nikasome mchepuo wa HGk masomo hayo yote nina C yaani histori C geograph C na kiswahili C vipi inawezekana kuendelea?

    ReplyDelete
  11. Mimi naitwa juma nimehitimu kidato cha nne mwaka 2020 na kupata ufaulu wa daraja c ya 24 nahitaji kusoma kidato cha tano na cha sita kwa mwaka mmoja je inawezekana?,na Kama inawezekana ada itakuwa shilingi ngapi za kitanzania?

    ReplyDelete
  12. Mm ni mhtimu wa astashahada ya ualimu naitaji kupata kituo Cha kufanya mtihani wa kidato Cha nne na utaratibu ukoje naomba msaada






    ReplyDelete