Saturday, November 22, 2014

UTARATIBU WA KUTUNUKU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE NA CHA SITA KWA KUTUMIA MFUMO WA GPA

MFUMO WA WASTANI WA POINT (Grade Point Average - GPA)
1. Huonesha wastani wa pointi alizopata mtahiniwa katika masomo aliyofaulu katika mtihani wake. 2. GPA hutokana na masomo saba (07) aliyofaulu vizuri zaidi mtahiniwa katika Mtihani wa Kidato cha Nne na masomo matatu (03) ya tahasusi katika Mtihani wa Kidato cha Sita. Mtahiniwa aliyefanya masomo pungufu ya 07 kwa CSEE au pungufu ya 03 kwa ACSEE, atafaulu  katika kiwango cha “Pass” endapo atapata angalau Gredi D katika masomo mawili au gredi C, B, B+ au A katika somo moja.
3. Uzito wa Gredi A= 5, B+ = 4, B = 3, C = 2, D = 1, E = 0.5 na F = 0.
4. Utaanza kutumika kupanga madaraja ya ufaulu katika Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2014 na Kidato cha Sita (ACSEE) 2015.

UKOKOTOAJI WA GPA YA MTAHINIWA
1. Hufanyika kwa kuchukua jumla ya uzito wa gredi katika masomo saba (07) aliofanya vizuri kwa Mtihani wa Kidato cha Nne na matatu (03) ya tahasusi kwa Mtihani wa Kidato cha Sita na kugawanya kwa idadi ya masomo.
Ukokotoaji  huo huzingatia kanuni ifuatayo:

                                Jumla ya Uzito wa gredi za masomo
         GPA  =        ------------------------------------------------
                                             Idadi ya Masomo

2. Masomo yatakayotumika katika ukokotoaji wa GPA ya mtahiniwa ni yale ambayo amefaulu; yaani amepata Gredi A, B+, B, C au D.

Mfano: Mtihani wa Kidato cha Nne, mtahiniwa aliyepata ufaulu wa Civics (A), History (B+), Geography (B+), Kiswahili (B), English (C), Physics (C), Chemistry (C), Biology (C) na Mathematics (E) atakuwa na jumla ya pointi 22 kwenye masomo saba aliyofanya vizuri. Idadi hiyo ya pointi ikigawanywa kwa idadi ya masomo saba (07), Mtahiniwa huyu atakuwa na Wastani wa Pointi (GPA) 3.1 na atatunukiwa daraja la Merit.
Katika Mtihani wa Kidato cha Sita mtahiniwa aliyepata ufaulu wa Physics (A), Chemistry (B+), Biology (A), Basic Applied Mathematics (D) na General Study (A) atakuwa na jumla ya pointi 14 kwenye masomo ya tahasusi (PCB). Idadi hiyo ya pointi ikigawanywa kwa idadi ya masomo matatu (03), mtahiniwa atakuwa na Wastani wa Pointi (GPA) 4.7 na atatunukiwa daraja la Distinction.

 MANUFAA YA KUTUMIA MFUMO WA WASTANI WA POINTI (GPA);
Ÿ1. Kuwa na mfumo wa kutunuku matokeo wa aina moja katika ngazi zote za mafunzo kuanzia Elimu ya Msingi hadi Elimu ya Juu;
2. Matokeo yaliyo katika mfumo wa wastani wa pointi kwenye cheti yatarahisisha kazi ya udahili wa watahiniwa unaofanywa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) katika ngazi za juu za mafunzo.
3. Mfumo wa wastani wa pointi (GPA) ni rahisi kueleweka kwa wadau wa kada mbalimbali kwa sababu hutoa tafsiri yenye kuonesha mtahiniwa aliye na GPA kubwa ndiye aliye na matokeo mazuri kuliko aliye na GPA ndogo.


Kwa maelezo zaidi kuhusiana na utaratibu huu BONYEZA HAPA

AU tembelea tovuti ya baraza la mitihani la taifa Tanzania www.necta.go.tz

Monday, September 1, 2014

SECOND SELECTION KIDATO CHA TANO 2014

UCHAGUZI WA WANAFUNZI KIDATO CHA TANO 2014 AWAMU YA PILI PAMOJA NA JOIN INSTRUCTION ZA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI MKUU
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano 2014 awamu ya pili.
Wanafunzi  8,101  wamechaguliwa  kujiunga  na  kidato  cha  tano awamu  ya  pili  2014,
kati  ya hao  4,987  wamepangwa  tahasusi  za sayansi  ya  jamii  na  biashara  na  wanafunzi  3,114 wamepangwa tahasusi za sayansi.

Aidha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shule ya sekondari Mkuu ni wanafunzi 30, ikiwemo kati yao wanafunzi 6 ni wasichana, na 24 ni wavulana. 
Wanafunzi hao wamechaguliwa kusoma tahasusi mbalimbali za Sayansi ya jamii (yaani HGK, HGL, HGE, EGM) na sayansi asilia (yaani PCM, PCB, CBG)
Wanafunzi  hawa  wanatakiwa  kuripoti  kwenye  shule walizopangiwa  kuanzia  tarehe  01 Septemba,  2014  na  mwisho  wa kuripoti ni tarehe 15 Septemba, 2014.


au





Imetolewa na Mtaaluma Mwandamizi
OFISI YA TAALUMA - SHULE YA SEKONDARI MKUU
31/08/2014

Wednesday, August 6, 2014

MATOKEO YA KIDATO CHA SITA (ACSEE 2014) YENYE MAJINA

Matokeo ya kidato cha sita Mkuu Secondary School, center number S0544 ni mazuri kulingana na idadi kubwa ya wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani hiyo. 

Wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani ni 206, ikiwemo Wasichana 62 na wavulana 144. Wanafunzi waliofanya mtihani ni 202, wanafunzi hao wamegawanyika katika tahasusi za HGL, HGE, EGM, CBG, PCB na PCM. 
Wanafunzi ambao hawakufanya mtihani huo kwa sababu mbalimbali ni wanne (4). 

Kwa ujumla matokeo ni kama ifuatavyo:
DIV-I = 10,    DIV-II = 44,    DIV-III = 100,    DIV-IV = 44,    DIV-0 = 1.

Kwa matokeo hayo, Jumla ya wanafunzi waliofaulu ni 198 sawa na asilimia 98.01%. Shule imeshika nafasi ya 23 katika shule 31 za mkoa wa Kilimanjaro zenye wanafunzi zaidi ya 30. Na vilevile imeshika nafasi ya 203 katika shule 268 zenye wanafunzi zaidi ya 30 nchini Tanzania.

Masomo matatu yaliofaulisha vizuri ni 
1. Economics
2. History
3. English Language. 

Wanafunzi 10 waliofanya vizuri zaidi (waliopata division I) ni:
1. HAGAI YONAH
2. DEOGRATIUS MLOWOLA
3. DAVID MORY
4. SANG'UNDI NKULUMU
5. STEPHANO DOMINICK
6. DIANA MLILO
7. FESTO EUGEN
8. SAIGURAN KORDUNI
9. JACKLINE MINJA
10. GILIAD MAKATA

Mwanafunzi aliefanya vibaya zaidi (Division 0) ni:
1. EMMANUEL MASSAWE

Kupata matokeo ya wanafunzi wengine wote yakiwa na majina Bonyeza HAPA

Tuesday, July 8, 2014