Wednesday, December 14, 2022

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA KWA MWAKA 2023

 πŸ“ŒKuona orodha ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza, bonyeza link hapa chini πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡





πŸ’₯Kupata fomu za kujiunga na shule mbalimbali (join instructions) bonyeza link hapo chini πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡






πŸ“’KUPATA FOMU YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI MKUU, BONYEZA LINK HAPO CHINI: πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡




Thursday, June 18, 2020

JOIN INSTRUCTION NA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO MWAKA 2020


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA UALIMU NA VYUO VYA ELIMU YA UFUNDI MWAKA, 2020

Jumla ya wanafunzi 121,251 wakiwemo wasichana 53,829 na wavulana 67,422 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, Vyuo vya Ualimu, na Vyuo vya Elimu ya Ufundi vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE). Idadi hii ni sawa na asilimia 93.4% ya wanafunzi wenye sifa za kuchaguliwa.

Wanafunzi wa Kidato cha Tano:  

Wanafunzi wote wa bweni waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2020 wanatakiwa kuripoti shuleni tarehe 18 Julai, 2020 tayari kwa kuanza masomo tarehe 20 Julai 2020
Aidha, wanafunzi wa kutwa waripoti na kuanza masomo tarehe 20 Julai 2020. Wanafunzi ambao hawataripoti wiki mbili tangu tarehe ya kufungua shule nafasi zao zitachukuliwa na wanafunzi wengine ambao hawakupangiwa shule katika awamu hii.
Uhamisho wa shule utaruhusiwa baada ya kukamilika kwa Muhula wa Kwanza wa masomo, na zoezi hilo litafanyika kwa kuzingatia uwepo wa nafasi kwenye Shule kwa
idhini ya Maafisa Elimu wa Mikoa husika. Hivyo, hakutakuwa na fursa ya kufanya mabadiliko yoyote ya Shule kwa sasa ngazi za Mikoa Halmashauri na shule.

Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Ufundi:

Wanafunzi waliopangwa kwenye Vyuo vya Elimu ya Ufundi vilivyopo chini ya NACTE wanatakiwa:
πŸ‘‰ Kuthibitisha kukubali kujiunga na kozi zinazosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) baada ya siku saba (7) kuanzia siku ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi hadi tarehe 15 Agosti, 2020.
πŸ‘‰ Mwanafunzi atafanya uthibitisho kupitia kiunganishi kinachoitwa Uthibitisho TAMISEMI katika tovuti ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ambayo ni www.nacte.go.tz ili kukubali kuchaguliwa kwenye kozi na vyuo walivyopangiwa.
πŸ‘‰ Mwanafunzi ambaye hatathibitisha kukubali nafasi aliyochaguliwa, nafasi yake itachukuliwa na wanafunzi wengine wanaoendelea kuomba katika Vyuo hivyo kwa njia ya mtandao.
πŸ‘‰ Wanafunzi wanaotaka kufanya mabadiliko ya kozi au chuo walikochaguliwa, wanaruhusiwa kufanya hivyo kuanzia tarehe 01 Agosti hadi 30 Agosti, 2020 kupitia mtandao wa NACTE.
πŸ‘‰ Vyuo ambavyo vimepangiwa wanafunzi, vitapata orodha ya waliochaguliwa kutoka NACTE kwa njia ya Mfumo (kupitia Institution Pannel) baada ya muda wa kuthibitisha na kuhama kukamilika.
πŸ‘‰ Maelekezo ya namna ya kuwasajili wanafunzi watakaoripoti Vyuoni kuanza masomo yatatolewa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).
πŸ‘‰ Wanafunzi waliopangwa katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya hawatahusika na utaratibu wa kubadilisha wa NACTE, hivyo wanapaswa kuwasiliana na vyuo husika.

Monday, June 18, 2018

SELECTION NA FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO MWAKA 2018

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2018 wataanza muhula wa kwanza tarehe 16 Julai, 2018. Wanafunzi wote wanapaswa kuripoti katika Shule aliyopangiwa kwa muda uliopangwa. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya mwisho ya kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.

Aidha, wanafunzi waliopangwa kwenye Vyuo vya Elimu ya Kati inabidi kufanya UTHIBITISHO kuanzia tarehe 17 Juni, 2018 hadi ifikapo tarehe 8 Agosti, 2018 wa kukubali kujiunga na Kozi na Vyuo walivyopangiwa kwa njia ya mtandao. Uthibitisho huo utafanyika kupitia tovuti ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ya www.nacte.go.tz katika kiunganishi kinachoitwa Uthibitisho OR-TAMISEMI 2018. Mwanafunzi atakayeshindwa kuthibitisha kozi na chuo alichopangiwa, nafasi yake itachukuliwa na wanafunzi wengine.
Mwanafunzi atakayetaka kufanya mabadiliko ya kozi na chuo alichopangiwa ataruhusiwa kufanya hivyo kuanzia tarehe 9 Agosti, 2018 hadi 23 Agosti, 2018 kupitia tovuti ya NACTE ya www.nacte.go.tz.

  πŸ‘‰BONYEZA HAPA KUONA ORODHA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO NA VYUO 2018

πŸ‘‰BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD JOIN INSTRUCTIONS ZA SHULE MBALIMBALI

πŸ‘‰BONYEZA HAPA KUPATA JOIN INSTRUCTION YA SHULE YA SEKONDARI MKUU 2018<<>>CLICK HERE TO DOWNLOAD MKUU SECONDARY SCHOOL JOIN INSTRUCTION 2018<<


  >>TAARIFA KWA UMMA - UCHAGUZI WA WANAFUNZI KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA UFUNDI NA VYUO VYA ELIMU YA KATI KWA MWAKA 2018


πŸ‘€Angalia Orodha ya Wanafunzi Wote Waliochaguliwa Tanzania bara===

Friday, February 9, 2018

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017 (CSEE 2017 RESULTS)


Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) Uliofanyika Novemba 2017 leo tarehe Januari 30, 2018. ambapo kiwango cha ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7 ukilinganisha na mwaka 2016.

Akitangaza matokeo hayo mbele ya waandishi wa habari, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo,  Dk Charles Msonde ameeleza kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 7.22 huku watahiniwa 265 wakifutiwa matokeo kwa udanganyifu wakiwemo wanafunzi 136 waliofanya mtihani wa kujitegemea (Private Candidate) na 129 waliofanya mtihani wa shule (School Candidate).

“Jumla ya Watahiniwa 287,713 ambao sawa na asilimia 77.09%  kwa shule za kawaida na vituo vya kujitegemea wamefaulu ambao katika ya hao wasichana wapo 143,728 sawa na asilimia 75.21% wakati wavulana wapo 143,985 sawa na asilimia 79.06%".

Shule kumi (10) Bora kitaifa ni kama ifuatavyo:
1.   St Francis Girls  - Mbeya
2.   Feza Boys - Dar Es Salaam
3.   Kemebos - Kagera
4.   Bethel Sabs Girls - Iringa
5.   Anwarite Girls - Kilimanjaro
6.   Marian Girls - Pwani
7.   Canossa - Dar Es Salaam
8.   Feza Girls - Dar Es Salaam
9.
   Marian Boys - Pwani
10. Shamsiye Boys - Dar Es Salaam

Shule kumi (10) za mwisho kitaifa:
1.   Kusini – Kusini Unguja
2.   Pwani Mchangani – Kaskazini Unguja
3.   Mwenge S.M.Z – Mjini Magharibi
4.   Langoni - Mjini Magharibi
5.   Furaha – Dar Es Salaam
6.   Mbesa – Ruvuma
7.   Kabugaro – Kagera
8.   Chokocho – Kusini Pemba
9.   Nyeburu – Dar Es Salaam
10. Mtule – Kusini Unguja











Monday, January 8, 2018

MATOKEO KIDATO CHA PILI NA DARASA LA NNE 2017 YATANGAZWA

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa darasa nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba 2017 mwaka jana, huku idadi kubwa ya wanafunzi wakifanya vyema katika mitihani hiyo.

Akitangaza matokeo hayo leo Jumatatu Januari 8, Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk Charles Msonde amesema jumla ya wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne wamefaulu  kati ya 1,158,444 waliofanya upimaji huo.

Amesema  wanafunzi hao wamefaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D wakati wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni ufaulu usioridhisha.

Kuhusu matokea ya upimaji wa kidato cha pili, Dk Msonde  amesema jumla ya wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa  kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea  na kidato cha tatu.


Dk Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili  51,807 sawa na asilimia 10.68 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.