Friday, December 29, 2017

WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2018 NA JOIN INSTRUCTION 2018

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akifafanua jambo wakati akiongea na Waaandishi wa habari kuhusu  matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 katika ukumbi wa Mikutano wa Tamisemi Mjini Dodoma.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amesema  kati ya wanafunzi 662,035 waliofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi  wanafunzi  650,862 sawa na asilimia 98.31 wamechaguliwa  kujiunga na  masomo ya kidato cha  kwanza katika awamu ya kwanza  mwaka 2018

Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 Tanzania Bara kwenye kikao na waandishi wa habari leo katika ofisi za Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Jafo amesema kuwa idadi wa wanafunzi   mwaka huu imeongezeka  kwa wanafunzi 124,209 ambapo ni sawa na asilimia  23.58 ikilinganishwa na wanafunzi 526,653 waliochaguliwa awamu ya kwanza kuingia kidato cha kwanza mwaka 2016.

Amesema kuwa wanafunzi 1912 wenye uhitaji maalum (pupils with special needs) waliofaulu mitihani ya darasa la saba  wamechaguliwa  kujiunga  na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2018 kwenye shule za sekondari za Serikali.

Mhe. Jafo amefafanua kuwa wanafunzi  11,173 sawa na asilimia 1.69 ya waliofaulu hawakupata nafasi ya kuchaguliwa  kujiunga  na kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza  ya uchaguzi  kutokana na uhaba  wa miundombinu ya elimu hususani  vyumba vya madarasa kwenye baadhi ya Halmashauri ya  Mikoa ya Lindi (170), Mbeya (3,092), Rukwa (4,091), Manyara (1,268), Katavi (976) na Simiyu (1,576).

Amesema kuwa Halmashauri ambazo zimeshindwa kuwapangia wanafunzi wote waliofaulu nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza ni Halmashauri za Lindi wanafunzi (80) Mbeya (207),Halmashauri ya  Jiji la Mbeya  ( 1,227), Mbarali (1,578),  Kalambo (166), Nkasi (1,318), Halmashauri ya Wilaya ya  Sumbawanga (1,054), Halmashauri ya Manispaa  ya Sumbawanga (1,553), Babati (581). Hanang (687), Mpanda (262), Nsimbo (714), Halmashauri ya Mji wa Bariadi (369) na Halmashauri ya Wilaya ya Busega (1,207).

Mhe. Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa ambayo haijakamilisha ujenzi wa miundombinu hasa ya vyumba vya madarasa  kuhakikisha wanakamilisha hadi kufikia mwezi februari, 2018 ili wanafunzi watakaochaguliwa kwenye awamu ya pili wapate nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018.

“Lengo la Serikali  ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba wanapata nafasi  ya kujiunga  na masomo ya kidato cha kwanza  nimeshatoa maelekezo  kwa wakuu wa mikoa kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapata nafasi  ya kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018” Amesema Jafo

Mhe. Jafo amesisitiza kuwa  walezi na wanafunzi ambao watakosa nafasi  katika awamu ya kwanza ya uchaguzi  kuwa wavumilivu wakati mikoa inajiandaa kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi wote kuanza na masomo ya kidato cha kwanza.

Amewaagiza  waalimu  na watendaji wa elimu  katika ngazi zote nchini kuongeza  bidii katika usimamiaji na ufuatiliaji wa utoaji wa elimu nchini na kushirikiana na wadau wa elimu  kukamilisha majengo na kuandaa mazingira  ya kuwapokea wanafunzi  wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza  2018 bila vikwanzao vikiwemo michango na ada ili  kutekeleza sera ya utoaji wa elimu  msingi bila malipo.

Aidha amewaomba Wazazi, Walezi na jamii kwa ujumla kushirikiana na Wilaya, Halmashauri na shule, kuhakikisha kwamba wanafunzi  wote waliochaguliwa wanaandikishwa , wanahudhuria na kubaki shuleni  hadi watakapohitimu  elimu ya Sekondari.


Sunday, June 11, 2017

Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha 5 na Vyuo vya Ufundi awamu ya Kwanza 2017

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha Tano Mwaka 2017


1.0 UTANGULIZI

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)
kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
imekamilisha zoezi la uchaguzi na upangaji wa wanafunzi wa kujiunga
na masomo ya Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi vya Serikali kwa
mwaka 2017 ambao walihitimu Kidato cha Nne mwaka 2016.
 

2.0 MATOKEO YA UFAULU KWA UJUMLA 
Jumla ya watahiniwa wa shule 349,524 wakiwemo wasichana 178,775sawa na asilimia 51.1 na wavulana 170,749 sawa na asilimia 48.9walifanya mtihani wa kumaliza Kidato cha Nne mwaka 2016. Watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani huo mwaka 2016 walikuwa 47,751 wakiwemo wasichana 24,587 sawa na asilimia 51.5 na wavulana 23,164 sawa na asilimia 48.5.Watahiniwa waliofaulu kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara. Hivyo ufaulu katika mwaka 2016 uliongezeka kwa asilimia 3.15ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2015.
 
3.0 TARATIBU ZA UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI KWA MWAKA 2017
Kwa mujibu wa mwongozo wa uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano, mwanafunzi anayeomba kuchaguliwa kuendelea na Elimu ya Sekondari ya Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi hulazimika kujaza fomu ya uchaguzi Selform ambayo ndiyo fomu rasmi ya maombi ya kuchaguliwa. Kwa kutumia fomu hiyo, mwanafunzi hujaza machaguo matano ya tahasusi (Combinations) za masomo anayotaka kusoma na Shule anayoipenda kujiunga nayo kwa kila chaguo.
Kwa kuzingatia utaratibu huo, Mfumo wa kieletroniki wa Uchaguzi hutumika kumpanga mwanafunzi katika machaguo yake ya masomo na Shule kwa kuanzia na chaguo la kwanza hadi la tano kulingana na kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi. Mfumo humpangia mwanafunzi chaguo la tahasusi aliyofaulu zaidi kuliko machaguo mengine.
Kwa mwaka huu 2017 Uchaguzi na upangaji wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi umezingatia mwongozo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wa tarehe 15 Mei, 2017. Mwongozo huu unaelekeza kwamba, kigezo cha mwanafunzi kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi ni;
i)
AAA hadi CCD kama cut off point kwenye masomo ya tahasusi
ii) Credit 3 na pointi zisizopungua
25 kwenye Daraja,
iii) Machaguo yaliyojazwa na mwanafunzi kwenye selform. 
iv) Nafasi zilizopo katika Shule husika
Napenda kusisitiza kwamba, vigezo hivi ndivyo vinavyotumika kwa mwanafunzi kujiunga Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka huu. Nia ni kuinua kiwango cha Elimu na Ujuzi kwa Elimu ya Juu Nchini.
 

4.0 WANAFUNZI WENYE SIFA ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO MWAKA 2017
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha Tano mwaka 2017wanatoka kwenye Shule za Serikali na zisizo za Serikali ambapo Shule351 zikiwemo shule 17 mpya zimepangiwa wanafunzi.
Kati ya wanafunzi 96,018 ni wanafunzi
93,019 ndio wenye sifa za kuchaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa kuwa wamefaulu vigezo vyote vya msingi kama nilivyoainisha hapo juu. Kati ya hao, Wanafunzi 92,998 ni wa Shule (School Candidates) na Wanafunzi 21walisoma chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima. 

 5.0 TAREHE YA KURIPOTI WANAFUNZI KATIKA SHULE WALIZOPANGIWA 
Muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano kwa mwaka 2017, utaanza tarehe 17 Julai 2017 lakini kwa wanafunzi wanaongia Kidato cha Sita watafungua Shule tarehe 3/7/2017 kama ilivyokuwa imepangwa. Kwa kuwa upangaji wa wanafunzi wanaoingia Kidato cha Tano kwa mwaka 2017 umezingatia machaguo ya wanafunzi wenyewe na nafasi zilizopo katika Shule husika, hakutakuwa na fursa ya kufanya mabadiliko yoyote ya Shule.Nitumie nafasi hii, kuwaagiza wanafunzi wote kuripoti katika Shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya kufungua Shule , nafasi yake itachukuliwa na wanafunzi wengine.
 

Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2017 inapatikana kwenye tovuti ya ORTAMISEMI ya: www.tamisemi.go.tz & www.moe.go.tz 
Aidha, fomu za kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi (joining instructions) zinapatikana kwenye shule alikopangiwa mwanafunzi na kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ya: www.tamisemi.go.tz





  

CLICK/BONYEZA HAPA KUPATA JOIN INSTRUCTIONS KIDATO CHA TANO 2017/18 >>>  
    







Wednesday, February 1, 2017

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2016


Barazala Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.

Katibu Mtendaji wa baraza la mitihani, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.

Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.

Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60.

Kwa upande wa masomo, amesema ufaulu katika masomo ya History, Geography, Kiswahili, English Language, Basic Mathematics, Physics, Biology, Commerce na Book keeping umepanda kwa kati ya asilimia 0.12 na 8.08 ikilinganishwa na mwaka 2015.

Somo lililoongoza kwa ufaulu ni Kiswahili ambapo asilimia 77.75 wamefaulu na somo la mwisho ni Basic Maths ambalo asilimia 18.12 ya watahiniwa wa shule wamefaulu.

Kati ya wanafunzi 10 bora kitaifa, wanafunzi 5 ni wasichana na 5 ni wavulana wakiongozwa na Alfred Shauri kutoka Feza Boys ya Dar es Salaam.

SHULE 10 BORA KITAIFA:
  1. Feza Boys Sec School – Dar es Salaam
  2. St. Francis Girls Sec School - Mbeya
  3. Kaizirege Junior Sec School – Kagera
  4. Marian Gilrs Sec School – Pwani
  5. Marian Boys Sec School - Pwani
  6. St. Aloysius Girls Sec School – Pwani
  7. Shamsiye Boys Sec School – Dar es Salaam
  8. Anwarite Girls Sec School - Kilimanjaro
  9. Kifungilo Girls Sec School - Tanga
  10. Thomas More Machrina Sec School – Dar es Salaam

SHULE 10 ZILIZOFANYA VIBAYA KITAIFA:
  1. Kitonga Sec School - Dar Es Salaam
  2. Nyeburu Sec School - Dar es Salaam
  3. Masaki Sec School – Pwani
  4. Mbopo Sec School – Dar es Salaam
  5. Mbondole Sec School – Dar es Salaam
  6. Somangili day Sec School – Dar es Salaam
  7. Dahani Sec School – Kilimanjaro
  8. Ruponda Sec School – Lindi
  9. Makiba Sec School – Arusha
  10. Kidete Sec School – Dar es Salaam
Kati ya shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa, shule 6 zinatoka katika mkoa wa Dar es Salaam wakati shule iliyoongoza ikiwa ni Feza Boys ya Dar es Salaam. Pia katika shule kumi bora kitaifa, hakuna shule ya serikali

Mkoa wa Njombe umeongoza katika mikoa 10 iliyofanya vizuri zaidi kitaifa ukifuatiwa na Iringa, Kagera, Kigoma na Kilimanjaro huku halmashauri za Bukoba Mjini, Njombe, Kakonko, Kahama na Wang'ing'ombe pia zikiibuka vinara.






********

Sunday, January 15, 2017

MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA PILI 2016

Baraza la Mitihani nchini – NECTA limetoa matokeo ya mitihani ya upimaji kwa wanafunzi wa kidato cha pili kwa wanafunzi wa shule za sekondari yanayoonesha ufaulu kuongezeka kwa 1.9%.

Katibu Mtendaji wa Baraza lza Mitihani nchini Dkt Charles Msonde ndiye aliyetoa taarifa hiyo jana jijini Dar es Salaam ambapo katika hali isiyo ya kawaida, shule tisa kati ya kumi zilizofanya vibaya katika mtihani wa kidato cha pili nchini, zimetoka mkoani Mtwara.

Amesema ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.9 kutoka 89.12% mwaka 2015 hadi kufikia 91.02% mwaka 2016 ambapo wanafunzi 372,228 wamepata alama zinazowawezesha kuingia kidato cha tatu huku wanafunzi 36,737 wakishindwa kufikisha alama hizo.

Shule ya St. Francis Girls ya Mbeya imeongoza katika shule 10 bora kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha pili mwaka 2016

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, idadi ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya I, II, na III ni 178,115 sawa na asilimia 43.55

Kuhusu ufaulu wa masomo, amesema, katika masomo ya Civics, History, Geography, Kiswahili, Phiysics, Chemistry, Chemistry, Biology na Basic Mathematics umepanda ikilinganishwa na mwaka 2015.

Aidha ufaulu kwa somo la English Language pekee ndio ambao umeshuka ikilinganishwa na mwaka 2015.

Somo lililofanyika vizuri zaidi ni Kiswahili ambapo asilimia 90.06 ya wanafunzi wote, wamefaulu na soko lenye ufaulu wa chini zaidi ni Basic Mathematics ambapo asilimia 21.55 wamefaulu.

Mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi ni Teckla Erasmo Haule kutoka Canosa ya Dar es Salaam akifuatiwa na Joseph Fabian Kalabwe wa Kwema Modern ya Shinyanga na Mirable Rayner Matowo wa Canosa ya Dar es Salaam.

Katika wanafunzi 10 bora kitaifa, wanafunzi 9 ni wasichana, na watano kati yao wanatoka Feza Girls.

Matokeo ya wanafunzi 31 yamefutwa baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu
.