Saturday, June 25, 2016

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO 2016

Ofisi ya Raisi-TAMISEMI imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2016. Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali.
Jumla ya wanafunzi 65,720 wakiwemo wasichana 29,457 na wavulana 36,263 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 34,064 wakiwemo wasichana 13,466 na wavulana 20,598 sawa na asilimia 52 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; na wanafunzi 30,897 wakiwemo wasichana 15,445 na wavulana 15,452 sawa na asilimia 47 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara na wanafunzi 759 wakiwemo wasichana 220 na wavulana 539 sawa na asilimia 1 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Ufundi.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2016 wataanza muhula wa kwanza tarehe 11 Julai, 2016 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya shule. Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 24 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi mwaka 2016 pamoja na fomu za kujiunga (joining instructions) inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Raisi-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz

Kuona majina yote ya waliochaguliwa BONYEZA HAPA (Majina yapo kwa PDF)

Kuona Majina ya Waliochaguliwa Kwenda Shule ya sekondari Mkuu BONYEZA HAPA (Majina yapo kwa PDF)

Kuona majina ya waliochaguliwa kutoka shule ya sekondaro Mkuu BONYEZA HAPA (Majina yapo kwa PDF)

Kupata Join instruction ya Mkuu Sekondari >>BONYEZA HAPA