Saturday, January 9, 2016

USAJILI WA WATAHINIWA WA KUJITEGEMEA KIDATO CHA SITA (ACSEE) 2017

Tunapenda kuwajulisha watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) mwezi MEI, 2017 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba; 

1. Kipindi cha usajili kwa watahiniwa wa Kujitegemea kitaanza tarehe 1 Julai hadi 30 Septemba, 2016 kwa ada ya Shilingi 50,000/= Aidha, watakaojisajili kwa kuchelewa yaani tarehe 01/10/2016 hadi tarehe 30/10/2016 watalipa Shilingi 65,000/= ikiwa ni ada ya kawaida pamoja na faini. 

2. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani kuchukua namba rejea (reference number) zinazotolewa bure na kufanya malipo ya ada ya mtihani katika ofisi za Posta tu. 

3. Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz kwani muda wa usajili hautaongezwa.

Shule ya sekondari Mkuu, ni kituo kwa watahiniwa wa kujitegemea wa Maarifa (QT), Kidato cha nne(CSEE) na kidato cha sita(ACSEE). Kituo hiki cha watahiniwa wa kujitegemea kinasimamiwa na Taasisi ya Elimu ya watu wazima (TEWW/IAE) chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Kituo kimesajiliwa kwa namba M0544 na P0544. Kituo kinatoa elimu kwa wanaohitaji  kuanzia muda wa jioni saa 9, kwani kituo hiki kina walimu bora na waliobobea katika kutoa elimu na ushauri kwa wale wanaorudia na kwa wale wanaojiendeleza.

Karibu/Karibuni sana katika Kituo cha Shule ya Sekondari Mkuu.
Ukifika, Ulizia mratibu wa Watahiniwa wa kujitegemea(PC), Au Mwalimu Tarimo au Mwalimu wa Taaluma. Utapata maelekezo ya namna ya kulipa ada ya mtihani na kujisajili, na kama utakuwa tayari basi utasajiliwa hapohapo. Endapo utapenda kujiunga kusoma katika kituo cha shule ya sekondari Mkuu, utapatiwa fomu ya kujiunga na kituo hiki.