Thursday, September 1, 2016

WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO AWAMU YA PILI (SECOND SELECTION) 2016

OR-TAMISEMI imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya Pili (Second Selection) kwa mwaka 2016. 

Jumla ya wanafunzi 3,918 wakiwemo wasichana 2,413 na wavulana 1,505 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wanafunzi ambao hawakuripoti awamu ya kwanza.

Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 1,864 wakiwemo wasichana 1,099 na wavulana 765 sawa na asilimia 47.58 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; na wanafunzi 2,054 wakiwemo wasichana 1,314 na wavulana 740 sawa na asilimia 52.42 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2016 wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili (31/08/2016) atakuwa amepoteza nafasi hii.

Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2016 inapatikana kwenye tovuti ya OR-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz

 
 BONYEZA HAPA KUONA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA AWAMU YA PILI



Saturday, June 25, 2016

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO 2016

Ofisi ya Raisi-TAMISEMI imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2016. Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali.
Jumla ya wanafunzi 65,720 wakiwemo wasichana 29,457 na wavulana 36,263 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 34,064 wakiwemo wasichana 13,466 na wavulana 20,598 sawa na asilimia 52 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; na wanafunzi 30,897 wakiwemo wasichana 15,445 na wavulana 15,452 sawa na asilimia 47 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara na wanafunzi 759 wakiwemo wasichana 220 na wavulana 539 sawa na asilimia 1 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Ufundi.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2016 wataanza muhula wa kwanza tarehe 11 Julai, 2016 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya shule. Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 24 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi mwaka 2016 pamoja na fomu za kujiunga (joining instructions) inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Raisi-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz

Kuona majina yote ya waliochaguliwa BONYEZA HAPA (Majina yapo kwa PDF)

Kuona Majina ya Waliochaguliwa Kwenda Shule ya sekondari Mkuu BONYEZA HAPA (Majina yapo kwa PDF)

Kuona majina ya waliochaguliwa kutoka shule ya sekondaro Mkuu BONYEZA HAPA (Majina yapo kwa PDF)

Kupata Join instruction ya Mkuu Sekondari >>BONYEZA HAPA

Saturday, January 9, 2016

USAJILI WA WATAHINIWA WA KUJITEGEMEA KIDATO CHA SITA (ACSEE) 2017

Tunapenda kuwajulisha watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) mwezi MEI, 2017 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba; 

1. Kipindi cha usajili kwa watahiniwa wa Kujitegemea kitaanza tarehe 1 Julai hadi 30 Septemba, 2016 kwa ada ya Shilingi 50,000/= Aidha, watakaojisajili kwa kuchelewa yaani tarehe 01/10/2016 hadi tarehe 30/10/2016 watalipa Shilingi 65,000/= ikiwa ni ada ya kawaida pamoja na faini. 

2. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani kuchukua namba rejea (reference number) zinazotolewa bure na kufanya malipo ya ada ya mtihani katika ofisi za Posta tu. 

3. Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz kwani muda wa usajili hautaongezwa.

Shule ya sekondari Mkuu, ni kituo kwa watahiniwa wa kujitegemea wa Maarifa (QT), Kidato cha nne(CSEE) na kidato cha sita(ACSEE). Kituo hiki cha watahiniwa wa kujitegemea kinasimamiwa na Taasisi ya Elimu ya watu wazima (TEWW/IAE) chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Kituo kimesajiliwa kwa namba M0544 na P0544. Kituo kinatoa elimu kwa wanaohitaji  kuanzia muda wa jioni saa 9, kwani kituo hiki kina walimu bora na waliobobea katika kutoa elimu na ushauri kwa wale wanaorudia na kwa wale wanaojiendeleza.

Karibu/Karibuni sana katika Kituo cha Shule ya Sekondari Mkuu.
Ukifika, Ulizia mratibu wa Watahiniwa wa kujitegemea(PC), Au Mwalimu Tarimo au Mwalimu wa Taaluma. Utapata maelekezo ya namna ya kulipa ada ya mtihani na kujisajili, na kama utakuwa tayari basi utasajiliwa hapohapo. Endapo utapenda kujiunga kusoma katika kituo cha shule ya sekondari Mkuu, utapatiwa fomu ya kujiunga na kituo hiki.