Saturday, January 10, 2015

USAJILI WA WATAHINIWA WA KUJITEGEMEA WA KIDATO CHA NNE NA MAARIFA(QT) 2015 UMEANZA

Katibu  Mtendaji  wa  Baraza  la  Mitihani  la  Tanzania  anawatangazia watu  wote  wanaotaka  kufanya Mtihani  wa  Kidato Cha Nne  (CSEE)  na Maarifa (QT)  Mwezi  Novemba  2015  kwamba usajili  umeanza  rasmi tarehe  01  Januari 2015.  
Watahiniwa  watakaojisajili  katika  kipindi  cha  kawaida  yaani  tarehe  01 Januari  2015  hadi  28  Februari  2015  watalipa  ada  ya  Shilingi  50,000/-  kwa wanaojisajili    mtihani  wa  Kidato  cha  Nne  (CSEE)  na  Shilingi  30,000/-  kwa wanaojisajili  mtihani  wa  Maarifa  (QT).  
Watahiniwa  watakaojisajili  kwa kuchelewa  yaani  kuanzia  tarehe  01  Machi  2015  hadi  tarehe  31  Machi  2015, watalipa  ada  ya  Shilingi  65,000/  kwa  Kidato  cha  Nne  na  ada  ya  Shilingi 40,000/- kwa mtihani wa Maarifa (ada pamoja na faini).

Kabla  ya  kujisajili  kwenye  mtandao  waombaji watapaswa kwenda kwenye vituo wanavyokusudia kufanyia mtihani kuchukua namba  rejea  (Reference  Number).   Wakuu  wote  wa  vituo  nchini wamekabidhiwa  namba  rejea  na  watazigawa  kwa  watahiniwa  tarajali  bila malipo.   Aidha  waombaji  watapaswa  pia  kulipa  ada  ya  mtihani  kwa  njia  ya Posta  au  M-Pesa  kabla  ya kujisajili  kwani  hakuna  mtahiniwa  atakayeweza kujisajili  bila  kulipa  ada  ya  mtihani.  Waombaji  wote  wazingatie  kwamba kipindi cha usajili kitafungwa rasmi tarehe 31 Machi 2015. (kwa maelezo zaidi kutoka baraza la mitihani la Tanzania, Bofya HAPA au tembelea www.necta.go.tz)

Shule ya sekondari Mkuu, ni kituo kwa watahiniwa wa kujitegemea wa Maarifa (QT), Kidato cha nne(CSEE) na kidato cha sita(ACSEE). Kituo hiki cha watahiniwa wa kujitegemea kinasimamiwa na Taasisi ya Elimu ya watu wazima (TEWW/IAE) chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Kituo kimesajiliwa kwa namba M0544 na P0544. Kituo kinatoa elimu kwa wanaohitaji  kuanzia muda wa jioni saa 9, kwani kituo hiki kina walimu bora na waliobobea katika kutoa elimu na ushauri kwa wale wanaorudia na kwa wale wanaojiendeleza.

Karibu/Karibuni sana katika Kituo cha Shule ya Sekondari Mkuu.
Ukifika, Ulizia mratibu wa Watahiniwa wa kujitegemea(PC), Au Mwalimu Tarimo au Makamu Mkuu wa Shule. Utapata maelekezo ya namna ya kulipa ada ya mtihani na kujisajili, na kama utakuwa tayari basi utasajiliwa hapohapo. Endapo utapenda kujiunga kusoma katika kituo cha shule ya sekondari Mkuu, utapatiwa fomu ya kujiunga na kituo hiki.




RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2015 HAIJABADILIKA

Baadhi  ya  watu  wamekuwa  wakitumiana  ujumbe  kwenye  mitandao  ya
kijamii  wenye kupotosha kwamba    Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
ametangaza kuwa    Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) 2015 utafanyika
kuanzia  tarehe  2  hadi  25  Machi  2015  badala  ya   tarehe  4  hadi  27  Mei
2015.  Aidha,  ujumbe huo  umetoa  sababu  kuu ya mabadiliko  ya ratiba ya
mtihani  kuwa  inatokana  na  mwingiliano  wa  ratiba  ya  Uchaguzi  Mkuu  wa
mwaka 2015 na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Baraza  la  Mitihani  la  Tanzania  linapenda  kuwafahamisha  watahiniwa  wa
Mtihani wa Kidato cha Sita  2015 na umma  kwa ujumla  kuwa taarifa  hizo  ni
za  UONGO  na  zinalenga  kuupotosha  umma  wa  watanzania.    Baraza
linapenda  kusisitiza  kuwa  ratiba  ya  Mtihani  wa  Kidato  cha  Sita  2015
HAIJABADILIKA  na  kwamba  Mtihani  huo  utafanyika  kuanzia  tarehe  4
hadi  27  Mei  2015  kama  ilivyopangwa  awali,  Baraza  la Mitihani  linaomba
wadau wazipuuze taarifa hizi zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii
kwa kuwa zina lengo la kupotosha umma.


Imetolewa na Afisa habari na uhusiano, Baraza la mitihani la Tanzania

Bofya HAPA kupata RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA ACSEE 2015